Taasisi ya Biblia na Utumishi

Changamoto ya Uongozi wa 'Ufanisi' Kanisani

Hatua 1 ya Semina za Uongozi kwa Kozi za Kanda


Leadership Challenge Workshop : Level 1 Competency Seminar

 

Yaliyomo:

 

1.             Uongozi ni nini?  (What is leadership?)

2.             Madhumuni ya semina hii ni nini? (Workshop objectives)

3.             Njia mbali mbali  za kujifunza mambo ya Uongozi  (How we learn about leadership)

4.             Uzoefu wako mzuri wa Uongozi ulikuwaje (Your own 'personal best' leadership experience).

5.             Changamoto yako itakayokuja siku za karibuni ni nini?  (Your next leadership challenge)

6.             Matendo matano ya Uongozi wa kipekee. (Five practices of extraordinary leadership)

7.             Kuwa mfano wa uongozi mzuri (Modeling the way)

8.             Mifano ya kiblia (Biblical examples of modeling the way)

9.             Kubainisha maadili yako (Clarifying you values)

10.        Tabia za viongozi waliosifiwa (Characteristics of   admired leaders)

11.        Kusawazisha matendo  na maadili yako. (njia za kufundisha maadili) (Align your actions and your values)

12.        Kutumia mafundisho ya 'mifano' ili kushinda kwenye changamoto ijayo. (Applying modeling to your next challenge)

13.        Kushirikisha maono kwa njia ya kutia moyo. (To inspire a shared vision).

14.        Mifano ya kibiblia. (Biblical Examples)

15.        Kutumia 'kushirikisha maono kwa njia ya kutia moyo' ili kufaulu kwenye changamoto  zako. (Applying 'Inspiring a shared vision' to your next challenge. Envision the future by imagining exciting and ennobling possibilities)

16.        Kukabili mila na desturi  (Challenging the process)

17.        Mifano ya Kibiblia  (Biblical examples)

18.        Kutofautisha msimamizi na kiongozi katika kazi mbali mbali. (Contrasting managers and Leaders in key functions)

19.        Kutambua viongozi na wasimamizi kanisani. (Applying the manager/leader grid)

20.        Kutumia 'kukabili mila na desturi' ili kufaulu kwenye changamoto yako ijayo.  (Applying 'Challenging the process' to your next challenge)

21.        Kuwawezesha wengine kutenda (Enabling others to act)

22.        Mifano ya Kibiblia (Biblical examples)

23.        Kuweza na kutoweza (powerful times /Powerless times)

24.        Kutumia 'kuwawezesha wengine kutenda' ili kufaulu kwenye changamoto yako ijayo. (applying 'Enabling others to Act' to your next challenge

25.        Kutia moyo (Encouraging the heart)

26.        Mifano ya Kibiblia (Biblical examples)

27.        Uzoefu wako wa pekee uliotambulika (Your most meaningful recognition)

28.        Kutumia 'kutia moyo' kwenye changamoto yako ijayo. (Applying 'Encouraging the Heart' to your next challenge)

 

 

 

1. Uongozi ni nini?

  

Kuna mifano au picha  mbali mbali ya uongozi katika kila utamaduni. Shirikisha mifano mitatu ya uongozi wa utamaduni wako.

  

 

Katika ufahamu wako Kiongozi  ni mtu wa aina gani, anafanya nini ili awe kiongozi ­­­­­­­­­­­­_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

A godly leader is one who influences a particular group of God's people towards God's purposes for the group'  Dr. J Robert Clinton

Kiongozi anayemcha Mungu ni mtu anayeweza kuwaelekeza kundi la watu wa Mungu ili  walielekee  kusudi la Mungu.

Text Box: Kiongozi     Text Box: Kundi    Text Box: kazi

 

Zaburi 78:72

 

2. Madhumuni ya Semina hii

 

 

Kusudi la semina hii ni kukusaidia kuboresha ustadi wako wa Uongozi ili kufanya kazi ya Mungu kwa Ufanisi.  Kwa hiyo kwa sababu ya semina hii utagundua mambo yafuatayo:

 

 •         Kuelewa uwezo na upungufu wako katika uongozi
 •         Kugundua wakati mwafaka kufanya kazi tofauti na uzoefu wako 'to take risks'
 •         Kukabili mila na desturi ili kufanya kitu kipya cha ufanisi
 •         Kujenga mahusiano mazuri kati ya wewe na Viongozi wenzako na Wakristo wenzako
 •         Kuendeleza zaidi maono yako kwa kazi ya Mungu mahali ulipo, na kuwajulisha mpaka watakapoyapokea na kuyamiliki maono haya
 •         Kujulisha maadili ya msingi kwa njia za matendo yako
 •         Kuwatia moyo Wakristo wako kufanikiwa na kushirikiana katika kazi ya Mungu.
 •         Kutambua mafanikio ya wengine

 

Ili kuona faida kubwa katika semina hii, orodhesha madhumuni matatu unayoyatarajia kufanikisha.

 

1._______________________________________________________________________

2._______________________________________________________________________

3._______________________________________________________________________

 

3.  Njia mbali mbali  za kujifunza mambo ya Uongozi  (learning cycle)

 

 

       
 
 
   

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

4. Uzoefu wako mzuri wa Uongozi ulikuwaje?

 

 

 

Katika mambo ya uongozi, inawezekana kwa uzoefu wako kukufundisha  zaidi kuliko walimu wote wengine. Viongozi wengi wanajifunza kwa njia za kujifanya wao wenyewe na kwa kuwaangalia wengine.  Kila mmoja wetu amewahi kufanikiwa angalau kipindi kimoja katika uongozi wake.  Mifano hii ni mifano ya Uongozi wa ufanisi.

 

Jaribu kumbuka kipindi ambacho ulikuwa kiongozi mzuri sana kanisani. Andika kwa kifupi mifano mitatu ya mafanikio yako kwa sentensi moja moja. K.m. ' Kuanzisha idara au kazi  mpya, au ulikuwa mwenyekiti mzuri kwenye kikao fulani, au ulifanikiwa katika kazi ya kutoa ushauri n.k.

 

1.________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

2________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

3________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

 

Sasa tafakari mambo haya matatu uliyoandika hapo juu.  Na katika nafasi ya chini orodhesha mambo ambayo yalikuwezeshwa kufanikiwa katika mambo hayo.  Ulifanyaje ili kufanikiwa katika kila kazi?

 

1________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

2.________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

3.________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

Sasa kutoka mambo haya matatu umeona masomo ya misingi ni nini kuhusu uongozi wako.

 

________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________Shirikisha mambo haya miongoni mwa watu kwenye kundi lako.

 

5.  Changamoto yako itakayokuja siku za karibuni ni nini ?

 

Tafakari sasa kuhusu uongozi wako na majukumu yako ya sasa.  Fikiri kuhusu mradi moja au hali moja ambayo inaleta changamoto.  Chukua kitu ambacho ni kikubwa zaidi, halafu andika jina lake hapo chini.

 

_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

Elezea chagamoto

 

_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

Orodhesha mambo au shida katika hali hii ambazo ni ngumu. (Dhumuni ni kubainisha mambo ya kutatua)

 

1.__________________________________________________________________________________________________________

2.__________________________________________________________________________________________________________

3.__________________________________________________________________________________________________________

4___________________________________________________________________________________________________________

 

 

6. Matendo matano ya Uongozi wa kipekee

 

Katika miaka 20 Jim Kouzes na Barry Posner wamegundua matendo matano ambayo viongozi wanafanya hapa duniani ili kuleta utendaji wa ufanisi. Mambo haya yametokea katika miaka 20 ya uchunguzi miongoni mwa viongozi ziadi ya 250,000.

 

Katika utafiti wao, Jim Kouzes na Barry Posner walidhamiria kugundua matendo ya kawaida ya watu wa kawaida yaliyoleta utendaji wa ufanisi. Katika kesi zote walizozichunguza waligundua 'Matendo Matano ya Utendaji wa Ufanisi'. (' The five practices of Exemplary Leadership'.)

 

1. Kuwa mfano wa uongozi mzuri (Modeling the way)

 

Viongozi kwa kawaida huanzisha kanuni kuhusu jinsi gani wanataka watu watendewe na pia malengo yafuatwe. Wanaazisha viwango vya hali ya juu kwa wengine kufuata. Kwa sababu watu wanaweza kushindwa katika matatizo ya utata, viongozi wanatayarisha malengo ya muda ili watu wao wafaulu katika kazi ndogo ndogo. Kazi hizi ndogo huchangia malengo makubwa. Viongozi wanabomoa urasimu katika kipindi ambacho kinazuia matendo. Kama watu wameshindwa kufanikiwa,  viongozi wanaonyesha njia za kufanya. Wanatengeneza nafasi za ushindi.

  

2. Kushirikisha maono kwa njia ya kutia moyo. (To

     inspire a shared vision).

 

Viongozi wanajiamini kwamba wanaweza kuleta tofauti.  Wanaweza kuona mbele, kuumba picha au mfano bora ya kanisa la kipindi kichajo. Kwa sababu ya karama zao wanaweza kuwavuta wengine ili kuamini maono yao. Wanawawezesha wengine kuona kwamba maono yao yanawezekana.

  

3. Kukabili mila na desturi  (Challenging the process)

     

Viongozi wanatafuta nafasi ya kubadilisha hali kama  ilivyo sasa. Wanatafuta njia za ubunifu ili kuboresha chama chao. Wale viongozi wanafanya jaribio ili kufanya kitu kipya na pia hata hivyo wanajua watakosea labda watashindwa katika mambo mbali mbali lakini wanajua - kuwa 'There is no gain without pain' (hakuna mapato bila maumivu'). Wale viongozi wanajua kwamba masikitiko haya ni nafasi ya kujifunza somo jipya.

 

4. Kuwawezesha wengine kutenda vizuri (Enabling

     others to act)

 

Viongozi wanaendeleza ushirikiano na wanajenga 'timu' au makundi yaliyo thabiti na hai. Kwa kusudi wanahusisha wengine. Viongozi wanaelewa kwamba kuheshimiana kwa pamoja ni kitu cha msingi ili kuendeleza matendo ya pekee; Wanajitahidi kuleta hali ya uaminifu na hadhi za binadamu. Wanaimarisha wengine mpaka wanajisikia  kuwa na uwezo mwingi wa jitihada.

 

5.  Kutia Moyo (Encouraging the Heart)

 

Ili kutekeleza matendo ya pekee kwenye makanisa yetu,  kazi ngumu zinahitajika. Kwa hiyo viongozi wanazitambua kazi za kila mtu kanisani. Katika kila kundi wajumbe wanahitaji kushirikiana katika mafanikio, viongozi wanasherekea mafanikio.

 

  

7. Tendo la kwanza :Kuwa mfano wa uongozi mzuri (Modeling the way)

 

Mwanzo 1 inatuambia kwamba Mungu alipopanga  uumbaji alisema ' Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu' (1:26) dhumuni lake lilikuwa kwa binadamu kufanana naye.  Kwenye Biblia tunaona kanuni hii ya 'kuwa mfano' kutoka kipindi cha wakubwa  wa familia, manabii. makuhani na wafalme. Katika Agano jipya tunaona jinsi Yesu mwenyewe alikuwa mfano kwa thenashara wake. ( Marko 3:14) Pia Mtume Paulo miongoni mwa marafiki zake.  (1 Wakorintho 11:1)

 

 

Ili kuwa mfano kwa wafuasi wako ni lazima uanze na:

 

1. Kubainisha maadili yako ya misingi (identify your core values)

2. Matendo yako yawe sawa na maadili yako

 

 

 

1-10

1

Ninaonyesha mfano mzuri kwa wengine

 

2

Ninatumia muda kuthibitisha kwamba watu wangu wanafuata kanuni na maadili ya Kanisa letu

 

3

Ninatimiza ahadi zangu zote.

 

4

Ninawaomba wengine kwa kunitathmini kuhusu matendo yangu na jinsi yanavyoathiri wengine

 

5

Ninajenga makabiliano ya maadili kwa kuendesha kanisa langu

 

6

Nafahamu falsafa ya Uongozi wangu

 

 

Kwa jumla

 

 

 Tabia ya muhimu sana zaidi kuliko tabia zote ambazo watu wanatafuta kwenye kiongozi ni kusadikika.  Kusadikika ni msingi wa uongozi wote. Kama watu hamwamini yule mjumbe (mchungaji /Mwinjilisti) hawawezi pia kuamni ujumbe wake.

Vyeo (kama Mch/Mwj/Mheshimiwa nk) vinapokelewa tu, lakini uongozi wa kweli unahitajika.

Viongozi wanabainisha maadili yao ya misingi  na wanatenda kama wanavyoamini.  Au kwa maneno mengine wao ni wenye uaminifu na uadilifu.

 Inapaswa viongozi wajue kanuni zao na maadili yao ya msingi. Halafu wanatafuta njia za neema ya kuwahusisha  wengine. Si kwamba wanakemea tu, (Hii ni tabia za chekechea)

Ni vyema kwamba kiongozi anajua jinsi ya kutoa hotuba, lakini kutoa hotuba au kuhubiri haitoshi. Viongozi wa kipekee wanajua wanaheshimwa kwa sababu ya matendo yao. Matendo na maneno yao ni sawa.  Kwa njia za matendo yao ya kawaida ya kila siku wanajenga maendeleo.

 Viongozi wa pekee katika uchunguzi wetu wanafanya mambo yafuatayo:

 

  

1. Walifanya kazi yao kwa bidii,

2. Walifanya kwa umadhubuti

3. Walifanya kwa ustadi/ufanisi/ujuzi

4. Walifanya kwa usikivu wa makini.

5. Walichukua muda ya kutembelea na kutembea na watu

6. Walifundisha maadili yao kwa njia ya kutoa hadithi

7. Walionekana kwa vipindi vya vigumu au mashaka

8. walitatua shida za watu kwa neema na nidhamu, na kwa kuuliza maswali.

 

  

8. Mifano ya Kibiblia

 

Nehemia 4-5.                                        Nehemia kama mfano wa Uongozi mzuri

1 Samweli 12.                                         Ni mfano wa uongozi katika kipindi cha 

                                            ufisadi na rushwa.

Wafilipi 4:9                                                          Maneno ya Mtume Paulo

 

 

9. Kubainisha maadili yako.

 

  

A. Je unataka kusifiwa kwa sababu ya maadili ya namna gani katika Uongozi wako wa Kanisa?

_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

B. Kwa jinsi gani unaonyesha maadili yako? Au maadili yako yanaonekana kwa vipi?

_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

Fikiria viongozi wawili waliokuwa wa kipekee hapa duniani, labda wameongoza au kusabibisha  chama, kanisa  au shirika lao kuwa na hali ya juu. Andika majina yao hapa chini upande wa kushoto na katika sehemu ya kulia, kando ya majina yao, andika kanuni au maadili yao unayoyasifia wewe.

 

Jina la Kiongozi

Kanuni/Maadili yao

1.

 

2

 

 

Sasa fikiria hali ya uongozi uliyokabiliana nayo . Ulitumia kanuni au maadili gani ili kukata ushauri/kufanya uamuzi. Tathmini uamuzi wako katika mitazamo ya maadili na kanuni zako.

Je kwa jinsi gani maadili yako yaonekana zaidi kipindi kingine?

 

Maadili

Matendo ya kuonyesha maadili

1.

 

 

 

 

2

 

 

 

 

 

 

 

 

10. Tabia za viongozi waliosifiwa.

 

Angalia orodha ya maadili ya kawaida hapo chini.Weka alama kando ya yale maadili yanayohitahijika katika mitazamo yako kwa viongozi.

 

1.      _____Mtu anayetamani kuendeleza maisha yake,na kuwa  

Mtu mkuu. Anafanya kazi kwa bidii.  (Ambitious)

2.      _____Mtu mvumilivu mwenye kuheshimu mawazo ya  

wengine.(Broad minded)

3.      _____Mtu ambaye anawajali wengine, anawapenda na kuwalea.

    (Caring)

4.      _____Mtu mwenye ufanisi/utalaam/ustadi (competent)

5.      _____Mtu mwenye ushirikiano (Cooperative)

6.      _____Mtu mwenye ushujaa /Ujasiri (courageous)

7.      _____Mtu wa kutegemewa/kutumainiwa/kuwajibika (dependable)

8.      _____Mtu mwenye ushupavu, dhamira, kujitoa, kuendelea

(determined)

9.      _____Mtu bila upendeleo, tayari kusamehe, mwenye busara,

(Fair-minded)

10. _____ Mtu ambaye anaweza kuona mbali, anajali mambo ya 

wakati ujao na mustakabali wake (Forward-looking)

11. _____ Mtu mwenye ukweli /mwadilifu/mwaminifu (Honest)

12. _____Mtu mwenye ubunifu

13. _____ Mtu anayejitegemea

14. _____ Mtu anayetia moyo, mchangamfu, mwenye nguvu.

(Inspiring)

15. ____ Mtu mwenye akili na mantiki, kufikiri (Intelligent)

16. ____ Mwaminfu. (loyal)

17. ____Mtu mwenye uzoefu na busara(Mature)

18. ____Mtu mwenye kiasi, anjitawala (self controlled)

19. ____Mtu ambaye ni mwazi (straight forward)

20. ____Mtu ambaye anasaidia sana wa kufariji. (supportive)

 

 

 

Tabia nne za juu (watu wa Mataifa)

Tabia nne za juu (kundi lako)

11            88%

 

10            71%

 

4              66%

 

14            65%

 

 

_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

______________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

 

11. Kusawazisha matendo  na maadili yako

 

  Jinsi kiongozi anavyotumia muda wake inaonyesha

  Kipaumbele chake cha msingi.

 •         Vikao/Ajenda
 •         Kukutana na viongozi wengine
 •         Tukio maluum

 

Matukio ya dharura/utata, inatoa nafasi ya kuonyesha  kwamba kanisa linatoa uamuzi kulingana na maadili yake.       

 •         Vipindi vya kufundisha
 •         Matendo yenye maana

 

 

Hadithi (story) zinawasaidia watu kufahamu maadili ya kanisa lako.

 •         Mifano
 •         Vielelezo
 •         Mithali

 

  Mawasiliano ni ya muhimu sana katika uongozi wako.

 •         Maswali
 •         Madhumuni ya kanisa ambayo yameandikwa.
 •         Lugha ambayo unatumia na wengine.

 

 

 

Alama na sherehe ni ya muhimu ili  kusisitiza maadili ya kanisa na kuimarisha utamaduni wa kanisa

 •         Kusherehekea

 

 

  Kazi ya watu zitambulike kanisani ili kutia moyo.

Shukrani nk.

 

 

Nini ni vipaumbele vitano vyako vya msingi?  Mambo ambayo ni ya muhimu sana zaidi kuliko vitu vyote vingine

 

 

1.______________________________________________________________________

2______________________________________________________________________

3______________________________________________________________________

4______________________________________________________________________

5______________________________________________________________________

 

Kama ni hivyo andika hapo chini kwa jinsi gani vipaumbele vyako ni sawa na matendo yako:

 

 

 

 

Matendo

Jinsi kiongozi anavyotumia muda

 

 

 

 

Jinsi unavyoitikia kati kati ya matukio ya dharura

 

 

 

 

Jinsi unavyofanya mawasiliano

 

 

 

 

Jinsi unavyowatia moyo.

 

 

 

 

Jinsi unavyotambua kazi zilizofanyika kanisani.

 

 

 

 

 

 

12.  Kutumia mafundisho ya 'mifano' ili kushinda kwenye changamoto ijayo

 

 

 

 

Fuata hatua hizi :

 

 1. Jitambue maadili yako ya misingi ?
  1. Kwa njia ya faragha na Mungu kila siku. Kipindi hiki ni nafasi ya kuongea na Mungu, kutafakari sana kuhusu changamoto na kusawazisha maadili yako na mapenzi ya Mungu
  2. Andika kwenye 'diary' yako mawazo na masomo ambayo unajifunza
  3. Andika kwenye karatasi moja maelezo kwa mtu mwingine. Labda unaenda safari ndefu kwa miaka mingi. Maelezo unayoandika ni kuwasaidia watu wanaobaki kufanya maumuzi kama ulivyofanya wewe mwenyewe. Kwa hiyo andika kanuni zako ambazo  zitawaongoza waliobaki.
  4. Kusanya hadithi mbali mbali ambazo zinaonyesha maadili.

 

 1. Sawazisha matendo na maadili yako
  1. Unafanyaje ili kuonyesha kwamba uko 'serious' (makini) kuhusu maadili yako.
  2. Utatumia njia zipi ili kuwavuta watu kuona maadili ya msingi
  3. Inakupasa kubadilisha nini maishani mwako ili matendo yako yawe sawa sawa na maadili yako
  4. Kwa njia gani utawatia moyo na kusaidia wengine kuwa mfano mzuri pia.

 

___________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

 

 

13 Tendo la pili : Kushirikisha maono kwa njia ya kutia moyo

 

 

 

'Worldview' utamduni wa Kibiblia inatambua sehemu inayoonekana na ile isiyoonekana. Biblia inafundisha mahusiano kati kati ya kila sehemu. Au kwa lugha nyingine mambo yanayofanyika kwenye sehemu ambayo hainaonekani inaathiri au inaleta matukio katika sehemu inayoonekana.

 

'Vision' au uwezo kuona wa mbele ni kama daraja kati kati ya hizi sehemu mbili.  Ni uwezo kuona mambo yasiyoonekana na kuwajulisha wengine mambo Mungu mwenyewe anayotaka kufanya hapa duniani.

 

Viongozi wanaomcha Mungu huwasaidia wengine kuona makusudi na madhumini ya Mungu ili wao wenyewe wanahusishwa katika utekelezaji wake.

 

Ili kufanya hivi inapaswa kwa kiongozi kufanya mambo yafuatayo:

 

 

a.     Kuhisi/kuona wakati ujao kwa njia ya kutafakari mambo yanayowezekana.  K.m. itabidi tufunye hivi......

b.     Kuwashirikisha wengine katika mitazamo hii.

 

 

 

1-10

1

Kwa kawaida ninaongea kuhusu njia za kuboresha kazi

 

2

Ninaweza kuwaelezea wengine wakati ujao utakavyokuwa

 

3

Ninawaonyesha wengine kwamba wanaweza kufaulu wakishirkiana katika maono yao pamoja

 

4

Ninaweza kuchora picha kimawazo ya jambo tunalolitaka kufanya pamoja

 

5

Ninajenga makabiliano ya maadili kwa kuendesha kanisa langu

 

6

Ninasema kwa kuamini kabisa dhumuni na kusudi la kazi yetu kwamba ni la Mungu

 

 

 

 

 

Viongozi wa kipekee wanavutwa na mambo ambayo yataonekana kwa wakati ujao lakini bado hayajafanyika bado. Halafu wanaweza kukusanya watu kutimiliza maono yao.

 

Viongozi wanaona mbele na kutafakari mambo yanayowezekana. Wanajiamini (kwa msaada wa Mungu) wanaweza kuleta tofauti . Wanataka kuboresha hali ilivyo sasa iwe nzuri zaidi baadaye.

 

Lakini kuwa kiongozi ni lazima watu wakufuate. Ili kubadilisha maono yako kuwa maono yetu ni ishara kubwa wewe ni kiongozi.

 

Ili kuwavuta watu wengine ambao watasema "maono yako ni maono yetu" inapaswa kuwafahamu  na kuelewana. Inapasa wamwini kiongozi wao wakihusishwa na mitamazo yake. Katika lugha yake kiongozi na jinsi alivyoamini, wao watavutwa ili kuboresha hali zao.

 

14. Mifano ya Kibiblia

 

 

 

Kumbukumbu la Torati 28

Nehemia 2:17-18

Yohana Mtakatifu 16:12-24

 

 

 

 

 

15.  Kutumia 'kushirikisha maono kwa njia ya kutia moyo' ili kufaulu kwenye changamoto  zako

 

Maswali ya muhimu:

 

a.     Kwa jinsi gani unaweza kubainisha pamoja na wengine maono ya wakati ujao?

b.     Kwa jinsi gani unaweza kutabiri wakati ujao?

c.     Utafanya nini ili kupata msaada wa wengine kuhusu maono yako?

d.     Utafanyaje kuwasaidia wengine kuona mbele pia?

e.     Kwa vipi unaweza kushirikisha maono yako

f.        Kwa vipi unaweza kufanya zaidi na zaidi?

g.     Kwa jinsi gani unaweza kuboresha uwezo wako wa kukusanya watu kumiliki/kuhodhi maono yako?

h.     Utafanyaje kuwatia moyo ili wao wenyewe waweze kuwavuta wengine katika maono yako?

________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

16. Kukabili mifuatano ya mambo  (Challenging the process)

 

Mungu aliziumba mbingu na nchi na akaona ya kuwa  ni vyema. Lakini, binadamu walifanya dhambi ambazo zilisababisha uumbaji kuanguka katika  machafuko na upotovu. Mungu Katika Mwanzo 3 alichukua hatua mbali mbali ili kutatua hali hii na kuupatanisha uumbaji naye.  Kulinganisha na mpango na madhumuni ya Mungu, mara zote uongozi wa kumcha Mungu unachunguza hali ilivyo kuwa 'status quo' (hali kama ilivyo). Uongozi huu unatambua mambo ambayo hayajakamilika bado na  unashirikiana na Mungu ili kukamilisha au kusogeza hali ilivyo ili iwe karibu na mapenzi yake Mungu.

 

Mara kwa mara viongozi wanaomcha Mungu  wanakabili hali jinsi ilivyokuwa ili  kuwaingiza watu katika hali ilivyompendeza Mungu.

 

Maswali ya Muhimu:

 

 •                     Je, mara kwa mara tunatafuta njia za ubunifu ili kuboresha kazi zetu?
 •                     Kama tumeshindwa katika kazi fulani, je tunatumia nafasi ya kushindikana ili kujiuliza ' tumejifunza nini sasa'.(kutathmini)
 •                     Je tunapanga mipango inayowezekana, au tunapanga bila kufanya utafiti wa kutosha.

 

 

Kazi ya viongozi walivyompendeza Mungu ni kuleta mabadiliko, hawaridhiki katika hali ilivyo kuwa.  Mara kwa mara wanatafuta nafasi za kukua, kuboresha, kusogeza mbele.

 

Viongozi hawa wako tayari kupokea mitazamo na mawazo ya watu wengine na mahali pengine. Wajibu wao ni kukubaliana na mitazamo mizuri na kutafuta njia mbali mbali kutumia mitazamo hii ili kuleta mabadiliko.

 

Viongozi hawa wako tayari kutumia mambo mapya, hata wakishindwa. Wanajua mara kwa mara kuna kushindikana lakini badala ya kulaumu wanapojaribu, wanaanza tena na wanawatia moyo wengine ambao wanafanya hivi. Wanajua njia za kujifunza ni kufanya, hasa katika mazingira magumu.

 

Viongozi hawa wanatengenza mazingira ya mabadiliko, wanawasaidia wengine kufanya majaribio, hatua kwa hatua.

 

 

17.  Mifano ya Ki-Biblia

 

 

Nehemia 1-2

 

1 Samweli 17

 

Luka Mtakatifu 4:31-44.

 

 

 

 

 

18. Kutofautisha Wasimamizi na viongozi katika kazi mbali mbali. (Contrasting managers and Leaders in key functions)

 

Tofauti kati ya msimamizi na kiongozi ni nini?

 

Angalia tabia za msimamizi na kiongozi hapo chini.

 

 

Msimamizi

Kiongozi

 

1. Katika kazi ya kupanga: Msimamizi anaanzisha hatua za kina ili kufaulu. Anagawa rasmali ili kufaulu

1. Katika kazi ya kupanga: Kiongozi anaendeleza  maono kwa wakati ujao pamoja na mikakati ili kufaulu.

2. Katika kazi ya kuunda mtandao: Anaanzisha mifumo mbali mbali ya wafanyakazi, pamoja na sera na taratibu

2. Katika kazi ya kuunda mtandao: Anafanya mawasiliano kwa maneno na matendo ili kuanzisha timu zinazoelewa na kukubali maono na mkakati wa kanisa

3. Katika kazi ya utekelezaji: Anafuatilia matokeo, anatambua matokeo mazuri na mabaya. Anatoa sera na taratibu ili kutatua matokeo mabaya.

3. Katika kazi ya utekelezaji: Anawawezesha watu kushinda kwa kuwatia moyo

4. Katika kazi ya utekelezaji: Anaweza kutekeleza maazimio yote ya kamati.

4.  Katika kazi ya utekelezaji: Anasababisha mabadiliko yanayofaa.

 

 

19 Kutambua viongozi na wasimamizi kanisani.

 

Tambua viongozi wanne kanisani. Kutoka uzoefu wako je wanafanya kazi ya msimamizi ama kiongozi?

 

 

Jina

Kazi yake kanisani

Anafanya mambo ya uongozi au msimamizi

Afanye nini

1.

 

 

 

2.

 

 

 

3.

 

 

 

4.

 

 

 

 

 

 

20. Kutumia 'Kukabili mifuatano ya mambo'  ili kufaulu kwenye changamoto yako ijayo. 

 

 

1. Kwa njia gani mnaweza kuleta mabadiliko kanisani kwako?

  

2. Kanisa lako litaboreshwa mkifanya nini au mkibadilisha nini?

  

3. Kwa vipi mnaweza kuwasaidia wengine kupata nafasi za kukua kiroho na kubadilika.

 

4. Kuna mambo gani kanisani ambayo yanafanywa bila maana au sababu nzuri za kufanya. Au kwa lugha nyingine, sababu za kuanzisha mambo ambayo hayapo sasa = mambo mapya.

 

5. Kwa sehemu au kwa njia gani kanisani mnaweza kuanzisha kitu kipya  ?

 

6. Mmefanya kosa gani siku za karibuni katika kazi ya uongozi. Mmejifunza nini kutoka kosa lile. Je mmepata nafasi ya kuzungumzia kosa lile na wengine?

 

7. Kwa njia gani mnaweza kufahamu mambo yanayoathiri kanisa lako.

 

  

21 Kuwawezesha wengine kutenda (Enabling others to act)

Ile hadithi ya uumbaji wa binadamu katika Mwanzo 2 inaonyesha kwamba halikuwa lengo la Mungu kwa Adamu kuishi  peke yake na kutegemea nguvu zake tu.  Alipewa mke ili kumsaidia katika maisha yake.   Tunaona kama kivuli  katika Agano la Kale, lakini katika Agano Jipya, Yesu  alionesha kwa wazi umuhimu wa kutegemea nguvu za Roho Mtakatifu.  Vile vile kanisa au mwili wa Yesu tusiishi kwa uwezo wetu wenyewe, lakini kwa nguvu ya Roho wa Mungu.  

Roho Mtakatifu anatuwezesha  kufanya mapenzi ya Mungu na kufaulu katika kazi yake Mungu.

Vile vile katika mahusiano yetu sisi kwa sisi tunawezeshana katika njia mbali mbali, kwa sababu Mungu ametuumba kwa kusudi hilo.

 

Kwa hiyo tufanye mambo mawili ili kuwezesha wengine:

 

1. Kuleta ushirikiano kwa njia ya kuwashirikisha wengine malengo na kujenga uaminifu.

2. Kuimarisha wengine kwa njia ya kushirikiana nao. 

 

 

 

 

1-10

1

Kwa kawaida ninajenga mahusiano mazuri miongoni mwa watu ninaofanya kazi nao

 

2

Niko tayari kusikiliza mitazamo ambayo ni tofauti na yangu

 

3

Ninawaheshimu wengine

 

4

Nina 'support' (kuunga mkono) maumuzi ya wengine

 

5

Ninawapa watu wangu uhuru katika mikakati yao ya kufanya kazi kanisani.

 

6

Ninahakikisha kwamba watu wanakua ki-stadi katika kazi zao kwa kujifunza mambo mapya.

 

 

  

Viongozi wanajua hawawezi kufanya peke yao, wanategemea nguvu za Mungu na wanategemea wengine.  Viongozi wanawawezesha wengine kwa kuleta ushirikiano mzuri na kuimarisha wengine.

 

Kipawa cha 'uwezeshaji' ni ustadi fulani ambao unawezesha 'timu' ya watu kufanya kazi ya ufanisi. Viongozi wanaoleta ushirikiano mzuri wanawawezesha watu wao kufanya kazi ya kipekee.

 

Chanzo cha ushirikiano ni uaminifu. Viongozi wanaleta hali ya uaminifu kanisani, wanaelewa kwamba kuheshimiana inaendeleza kazi ya kipekee. Kama watu wanajua kwamba chanzo cha uongozi ni ushirikiano mzuri ambao umejengwa juu ya uaminifu na ujasiri, wao wenyewe wanaweza 'to take risks' (kujiingiza katika madhara) kufanya kazi tofauti, kuleta mabadiliko, kuleta hali ya uhai kanisani.  Pasipo hali ya uaminifu, na ujasiri watu hawataki kufanya mambo mapya, wanabaki kama walivyokuwa zamani bila maendeleo.

 

Kujenga hali ambayo watu wataheshimiwa ni chanzo cha kuimarisha wengine. Hali hii inabadilisha watu kutoka hali ya kuwa wafuasi hadi kuwa viongozi wao wenywe, ambao wanaweza kufanya kazi ya ki-pekee.

 

Kazi ya viongozi ni kuwasaidia watu mpaka waweze, kusimama imara, hadi kufikia kiwango cha kufahamu zaidi zaidi na zaidi. Viongozi wa pekee ni watumishi. Wanatumia mamlaka yao kuwahudumia wengine wanawawezesha wengine kufanya, si kwa kushika mamlaka lakini kwa kuwapa wengine nafasi ya kufanya.

 

Kama watu wamewezeshwa  'empowered' nawe wanaweza kutumia uweza wao kufanya kazi ya kipekee.

 ____________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

  

22 Mifano ya Kibiblia

 

Nehemia 3-4.  Nehemia aliwawezesha watu wa Yerusalemu kujenga tena ukuta wa mji katika siku 52, kwa njia ya kuwapa kila kitu walichohitaji kwa kazi zao.

 

Mathayo 10. Yesu aliwawezesha wanafunzi wake na kuwatuma ili kufanya huduma

 

1-2 Timotheo na Tito:  Paulo aliwezesha Timotheo kutatua shida kanisani.

 

23 Kuweza na Kutoweza (powerful times /Powerless times)

 

Kumbuka kipindi ambacho uliwezeshwa na mwingine kufaulu kwa sababu ya maneno yake au matendo yako. Elezea mambo yalivyofanyika.

 

__________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

 

Kumbuka kipindi ambacho ulijisikia vibaya, kama mtoto aliyekemewa kwa sababu ya maneno au matendo ya mtu mwingine. Elezea mambo yaliyofanyika kukusababisha kujisikia kama hivyo. __________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

24 Kutumia 'kuwawezesha wengine kutenda' ili kufaulu kwenye changamoto yako ijayo.

  

Unaweza kufanya nini katika hali ya kuwaheshimu watu na kuanzisha hali ya kuheshimiana?

 

Kwa njia gani unaweza kuleta nafasi za kusoma kwa watu wako?

 

Kwa njia gani unaweza kuwainua watu wengine, kushirikiana katika mafanikio?

 

Kwa njia gani unaweza kuingiza watu kwenye mitandao mbali mbali ili kupata rasilimali (resources) unazohitaji.

 

Unaweza kushirikisha kazi gani kwa wengine kufanya ambazo zitawawezesha na wao pia.

 

Upatikanaji wa viongozi

 

Unaweza kufanya nini ili kujenga umiliki (ownership) wa kazi au miradi yako?

 

Kwa jinsi gani unaweza kujenga hali ya uaminifu kanisani, ili watu waweze kufanya pamoja  k.m Harambee nk.

 

  

25. Kutia moyo (Encouraging the heart)

 

Luka 3:22 'Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.' Maneno haya yalikuwa muhimu sana katika maisha ya Yesu.   Katika mwanzo wa barua zake Paulo aliyapongeza makanisa kwa sababu ya tabia zao.  Kuna watu ambao wanaogopa kuwapongeza watu kwa sababu labda ingesababisha kiburi.  Lakini kumbuka kwamba Mungu ni Pendo, na Mungu anatupongeza .

 

Ili Kutia moyo fanya mambo yafuatayo:

 

1.      Tambua kazi za watu kwa kuwapongeza mbele ya wengine

2.      Shangilia maadili na ushindi kwa kuanzisha hali ya ushirikiano mzuri.

 

 

 

1-10

1

Kwa kawaida ninawapongeza watu kwa kazi ambazo walifanya vizuri?

 

2

Katika malengo yangu, ninawaambia watu kuwa ninawaamini uwezo wao kwa kazi fulani.

 

3

Ninathibitisha kwamba watu wanapokea pongezi kwa sababu ya mafanikio katika miradi au huduma zetu

 

4

Ninawatambua wale watu mbele za wengine

 

5

Ninatafuta njia za kusherekea mafanikio ya watu

 

6

Ninawapongeza watu kwenye timu yangu

 

 

Inawezekana kwa watu kanisani kuchoka au kukata tamaa, hata kufikia hali ya kujaribiwa na kuanguka kabisa. Viongozi wanawatia moyo kwa njia ya kutambua kazi zao na kusherekea mafanikio yao. Matendo ya upendo huwafariji sana.  Viongozi wanaanzisha hali ya kusherekea mafanikio.

  

26. Mifano ya Kibiblia

 

Yoshua 1

 

1 Mambo ya Nyakati 11

 

Warumi 16

 

 27. Uzoefu wako wa pekee uliotambulika (Your most meaningful recognition)

 

 

Kumbuka kipindi ambacho ulitambulika kwa sababu ya kazi yako. Elelzea jinsi ulivyojisikia. Orodhesha mambo uliyofanya, na jinsi ulivyotambulika na mwingine.   Kwa nini ilikuwa kipindi cha maana katika maisha yako.

__________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________

 

  

28  Kutumia 'kutia moyo' kwenye changamoto yako ijayo. (Applying 'Encouraging the Heart' to your next challenge)

  

 1. Kwa vipi unaweza kuwazawadia (reward) watu wengine kwa mambo madogo madogo?

 

 1. Unatumia nafasi gani ili kufanya kazi hii?

 

 1. Kwa vipi unaweza kuwatia moyo wengine kufanya hivi pia?

 

 1. Fikiri kuhusu miaka mia moja katika historia ya AICT

 

 1. Unaweza kupanga nini ili kusherekea mafanikio ya wengine

 

 1. Unafanya nini ili kuwa mfano katika jambo hili?

 

_____________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________________